Saturday, January 13, 2018 Ahukumiwa Miaka Mitatu Jela kwa Kumtusi na Kumtisha Mkuu wa Wilaya Mahakama ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, imemhukumu mkazi wa mtaa wa barabara ya Mbutu, mjini hapa, Mohamed Ahmed (54) kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kutiwa hatiani kwa kumtishia na kumtolea lugha ya matusi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo. Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Elimajidi Kweyamba, alidai mahakamani hapo kwamba mshitakiwa, alitenda kosa hilo Januari 09, mwaka huu, saa 1:05 usiku katika maeneo ya barabara kuu ya lami ya Igunga mjini. Alidai kuwa mshitakiwa huyo alimtolea lugha ya matusi Mwaipopo wakati akitekeleza majukumu yake. Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Igunga, Ajali Milanzi, Kweyamba alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo wakati mkuu wa wilaya akitekeleza agizo la upandaji miti kama lilivyotolewa maelekezo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassani. Aidha, mwendesha mashtaka alidai kwamba katika kosa la pil...