Msanii wa Bongo Fleva Tanzania Sam wa Ukweli ameaga dunia
Msanii wa Bongo Fleva Tanzania Sam wa Ukweli ameaga dunia
Msanii wa Bongo Fleva, Salum Mohamed aliyetamba kwa jina la Jukwaani kama Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Juni 7, 2018.
Sam alitamba sana na kazi zake kama vile Sina Raha alioutoa katika ya mwaka 2009 na 2010, Usiniache, Lonely na Hata kwetu wapo.
Hapo kati kati alipotea mpaka mwishoni mwa mwaka 2017 alipoibuka na kibao kingine kwa jina Kisiki na baadaye mwanzoni mwaka huu wa 2018 akauachia Wimbo Ni Wewe.
Ingawa ni mtu wa Singida Sam wa Ukweli amekulia Kiwangwa jirani na mji wa Dar es Salaam ambako amelelewa na Bibi yake mzaa mama.
Kwa mujibu wa aliyekuwa Meneja wa msanii huyo, Abdulmalik Mohamed , mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam na mipango ya mazishi inaendelea katika eneo la Tandale lakini Maziko yatafanyika Alhamis hii Kiwangwa mkoani Pwani.
Aidha meneja huyo amesema chanzo cha kifo cha msanii huyo ni Malaria na UTI (Urinary Tract Infection) ya muda mrefu.
Sam alikuwa akiandaa nyimbo zake mpya kabla ya kuanza kusumbuliwa na Tumbo akiwa Studio.
Ameacha mke na mtoto mmoja wa kike.
ANGALIA INTERVIEW YA MWISHO YA SAM WA UKWELI HAPA KWENYE LINK YANGU UONE NA USISAHAU KUSUBSCRIBE
https://www.youtube.com/channel/UCjUJbwIcScvwgaNMMr4Jfcg
Comments
Post a Comment