FAIDA ZA KABICHI KWENYE MWILI WA BINADAMU

Napenda kuwashukuru wote ambao mmekuwa mkishiriki katika masomo yangu, sasa kupitia ukurasa wangu wa facebook utajifunza mboga za majani zina umuhimu gani mwilini mwako. Hakikisha unaungana nami facebook kwenye ukurasa wa Mkumbo healthcare products ili uendelee kupata elimu hii adimu ambayo imekuwa na shuhuda nyingi sana na inaweza kuokoa gharama zako nyingi sana katika kuokoa afya yako.Unaweza kualika na marafiki zako waweze kulike page hii ili wajifunze zaidi.
KABEJI
Kabeji ni miongoni mwa mboga za majani zenye uwezo mkubwa sana kukufanya uwe mwenye afya milele na milele. Mmea huu unajulikana kitaalamu kama Brassica oleracea na unaweza kupatikana katika rangi mbalimbali, Kijani,nyekundu au damu yam zee nk.
Ili uweze kujipatia viini vyote vya mboga hii tunashauri ule kama kachumbali na hata kama ukiamua kupika kidogo hakikisha unapika inakuwa karibia na mbichi hii itasaidia kutoangamiza viini lishe ndani ya mboga hii yenye faida kubwa mwilini mwako.
FAIDA YA KABEJI KIAFYA
1. Ina kiwango kingi cha ANT-OXIDANT (Viondoa sumu mwilini)
Mwili wa binadamu unapokuwa unazalisha nishati ya mwili kutengeneza sumu ambazo ni mabaki ya hewa ya oxygen zinapo ungana zinaitwa Free radicals. Na endapo hizi Free radicals zikiachwa katika mwili wako huanza kuangamiza seli za huweza kuzibadili seli hata kuwa kansa. Na mwili huwa unaviondoa sumu vyake makini lakini pale panapotokea pamekuwa na uzalishaji wa free radicals nyingi sana mwili unalemewa unahitaji msaada. Na hapo ndipo mwili wako unatakiwa kuupa msaada kupitia ulaji wa vyakula vyenye viondoa sumu kama kabeji. Kabeji ina viini vitatu vyenye nguvu kubwa kuwezesha kuondoa free radicals zote zinazopatikana kupitia Oxidation stress na hizi zinajulikana kama thiocyanates, lutein, zeaxanthin, isothiocyanates, na sulforaphane. Viini hivi na uwezo wake mkubwa zinafanya mboga aina ya kabeji kuwa yakipekee katika aina zote za mboga. Mbali na kufanya kazi hizo pia zinauwezo mkubwa wa kuondoa cholestrol/mafuta mabaya mwilini mwako na kuufanya mfumo wa damu usukume damu kwa ufanisi wa hali ya juu na kuishi mwenye afya.
2. Ina kiwango kingi sana cha vitamin K
Ni Zaidi ya asilimia 85 ya mahitaji ya kila siku ya vitamin K hutolewa na kabeji endapo tu ukiifanya kuwa mboga yake na upikaji wake ukazingatia maelezo yangu hapo juu. Vitamin K ina msaada mkubwa sana kuhakikisha presha yako ya damu inakuwa katika kiwango cha kawaida muda wote. Na ndio msaada mkubwa wa neva za fahamu kufanya kazi vizuri katika usafirishaji wa taarifa. Hivyo kwa wale wenye matatizo ya kusahau hovyo na kama unapenda kuzuia ugonjwa wa kusahau wa uzeeni (Alzheimer's disease). Pia ina kiwango cha vitamin C takribani asilimia 54 zaidi hata ya chungwa. Hivyo ina uwezo mkubwa wa kukupa madini haya na kuupa mwili wako uwezo mkubwa Zaidi wa kuondoa Free radicals (Sumu) mwilini mwako na pia husaidia kwa kiwango kikubwa kuwezesha seli nyeupe za damu kupambana na maambukizi kupitia kuongeza kinga ya mwili.
3. Ina kiwango Kingi cha Vitamin B6,Vitamin B5,Folic acid,Magnesium,Chuma (Iron),Phosphorus,calcium.
Vitamin B6 inauwezo mkubwa kurekebisha utendaji kazi wa neva za fahamu zako hasa za ubongo na kuufanya ubongo wako utulie na ina msaada mkubwa sana kwa watu wenye msongo wa mawazo na hasira za mara kwa mara.
Magnesium ndio msingi wa shughuli zote zinazo endelea mwilini mwako, kwani ndio madini yanayo fanya shughuli zote zifanyike katika kiwango stahiki na endapo ikipungua shughuli zote za mwili zinafanyika katika kiwango cha chini sana maana inaongoza Zaidi ya viendesha shughuli za mwili (Enzymes) 300. Hivyo utumiapo kabeji utafurahia shughuli za mwili kufanyika katika kiwango sahihi.
MATUMIZI KIAFYA
Kikombe kimoja cha chai cha kabeji iliyo katwa ina viwango vifuatavyo
-Wanga 5gm
-Sukari 3gm
-Fiber( Nyuzi) 2gm
-Protin 1gm
- Sodium 16gm
JINSI YA KUTUMIA
Unaweza kupata viini lishe ndani ya kabeji kwa namna kuu tatu
1. Supu ya nyama iliyo changanywa na kabeji
2. Kachumbari ya kabeji
3. Juisi ya kabeji
NAMNA YA KUANDAA KWA MATUMIZI
1. SUPU YA NYAMA NA KABEJI
MAELEKEZO
-Chukua kabeji yako kata kata vizuri kisha pima vikombe 2 vya kabeji iliyo katwa na kisha osha kwa maji ya uvugu vugu yaliyo changanywa na chumvi na vinegar (Kama huna vinegar usihofu) chukua baking power kijiko cha chai changanya na maji kisha osha ckabeji. Lengo ni kuondoa vimelea na dawa zilizo gandamana kwenye nta ya mboga za majani. Kisha weka mafuta yako olive oil au Alizeti kwenye kikaangio kisha dumbukiza mboga zako,kipande cha pilipili hoho. Acha dakika chache kisha ipua na changanya na supu yako na nyama au shushia na supu yako bila kuchanganya
Unaweza kuweka parachichi lako moja ambalo utachanganya kwenye mboga yako.
2. JUISI YA KABEJI NA MBOGA ZINGINE ZA MAJANI
Chukua mboga zako za majani
-Kabeji vikombe 2
-Spinach vikombe 2
-Sukuma wiki vikombe 2
-Tango 2
-Mdalasini vijiko 2
-Tangawizi vipande 2
Osha mboga zako vizuri kama nilivyo eleza hapo juu, kisha dumbukiza kwenye kikamua juisi mboga zako aina moja baada ya nyingine.
Blenda yako inatakiwa iwe na uwezo wa kutenganisha juisi yenye kiwango kingi cha viini lishe na kuweka pembeni mabaki mengine.
Baada ya hapo iweke juisi yako kwenye mtungi mrefu wa blenda yako kisha changanya vizuri kupata juisi aina moja.
Kunywa juisi yako glasi moja unaweza kumpatia na ndugu yako glasi moja.
Huruhusiwi kuweka sukari,Asali na tunda lolote katika juisi ya mboga za majani.
Tumia juisi hii kama kinywaji chako.
MTUMIE RAFIKI YAKO NA MWAMBIE AJUMUIKE NASI KATIKA UKURASA HUU KAMA ANATAKA KUISHI NA AFYA BORA. pia usisahau kushare post hii basi utabarikiwa sana.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUFUNGUA BLOG KWENYE BLOGGER

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2017 HAYA HAPA

FAIDA NA MAAJABU JUISI YA UBUYU