Mwili wa Mzee Majuto Kuagwa Karimjee Leo
- Get link
- X
- Other Apps
Mwili wa Mzee Majuto Kuagwa Karimjee Leo
Mwili wa msanii wa vichekesho Amri Athumani ' King Majuto' aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, utaagwa leo Agosti 9, 2018 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais wa shirikisho la filamu Tanzania , Simon Mwakifamba amesema, Mzee Majuto ataagwa kuanzia saa 8.00 mchana katika viwanja hivyo na saa 10.00 jioni atasafirishwa kwenda nyumbani kwake Tanga kwa mazishi.
“Taarifa ambayo tumewasiliana na familia ni kwamba, Mzee Majuto ndugu jamaa na marafiki watatoa heshima za mwisho na baada ya hapo mwili utaelpelekwa nyumbani kwake Tanga kwa ajili ya mazishi,” amesema Simon Mwakifamba
Kwa upande mtoto wa Mzee Majuto, Ashrafu amesema,ratiba kamili ya mwili wa Mzee Majuto ni kwamba asubuhi mwili utaandaliwa katika Hospitali ya Muhimbili na shughuli zote ndogo ndogo zitafanyika hapo, baada ya hapo mwili utapelekwa Karimjee kwa ajili ya kuagwa saa nane mchana," anasema.
Install Application ya ATILIO KIBUGA BLOG Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD
Rais wa shirikisho la filamu Tanzania , Simon Mwakifamba amesema, Mzee Majuto ataagwa kuanzia saa 8.00 mchana katika viwanja hivyo na saa 10.00 jioni atasafirishwa kwenda nyumbani kwake Tanga kwa mazishi.
“Taarifa ambayo tumewasiliana na familia ni kwamba, Mzee Majuto ndugu jamaa na marafiki watatoa heshima za mwisho na baada ya hapo mwili utaelpelekwa nyumbani kwake Tanga kwa ajili ya mazishi,” amesema Simon Mwakifamba
Kwa upande mtoto wa Mzee Majuto, Ashrafu amesema,ratiba kamili ya mwili wa Mzee Majuto ni kwamba asubuhi mwili utaandaliwa katika Hospitali ya Muhimbili na shughuli zote ndogo ndogo zitafanyika hapo, baada ya hapo mwili utapelekwa Karimjee kwa ajili ya kuagwa saa nane mchana," anasema.
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD
Comments
Post a Comment