Monday, December 11, 2017 Ado Shaibu : “Sijaona hoja yoyote ya maana ya kunifanya niondoke ACT” Ikiwa vuguvugu la kuhama kwa wanasiasa limepamba moto nchini, Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, amesema haoni hoja ya msingi itakayo mshawishi kukihama chama hicho. Ado aliyasema hayo Novemba 9, 2017 siku moja baada ya aliyekuwa Mgombea kiti cha Urais kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kupitia ACT ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa chama hicho, Mama Anna Mgwira kuhamia CCM, uamuzi alioutangaza kwenye Mkutano wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) uliofanyika mjini Dodoma. Ado alifunguka kuwa, katika kipindi cha wiki mbili zilizopita ambacho hakuwepo kwenye mitandao ya kijamii na kupatikana kwenye simu iliyozoeleka, kuna baadhi ya watu baada ya kurejea hewani, walimtumia jumbe zenye kuhoji kama ameshahamia CCM kutoka ACT. “Jibu langu kwao lilikuwa jepesi. Siasa halisi si mzaha Kama mchezo wa komborera. Kwamba Leo ujifiche hapa kes...
Comments
Post a Comment