Monday, December 18, 2017 Dk. Kigwangalla Afunga Mafunzo Ya 15 Ya Jeshi USU Kwa Maafisa Wanyamapori Wa Tawa, Tanapa Na Ngorongoro Mkoani Katavi WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewaagiza wahifadhi wote nchini kushirikiana na wadau wengine hasa mamlaka za Mikoa na Wilaya katika maeneo yenye uvamizi wa mifugo na migogoro ya mipaka ya hifadhi ili kutatua changamoto hizo kwa namna shirikishi ikiwa ni pamoja na kuimarisha utoaji wa elimu kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo. Ametoa agizo hilo Disemba, 16, 2017 katika Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wakati akifunga mafunzo ya 15 ya mabadiliko ya kuelekea mfumo wa Jeshi Usu kwa Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa – TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro. “Kazi ya ulinzi wa rasilimali zetu za asili ni yetu na tutaiendeleza, Falsafa yetu ni kuwashirikisha wadau wote, kama kuna taasisi za kiraia kwenye ...
Wednesday, December 27, 2017 CCM yamjibu Askofu Kakobe baada ya kuikashifu serikali Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema Askofu Zakaria Kakobe wa Kanisa la FGBF lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam amekosa hekima na busara kwa kugeuza madhabahu ya kanisa kuwa jukwaa la kisiasa na kuanza kukashifu viongozi wa serikali akiwemo Rais Dkt John Pombe Magufuli. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, Frank Kamugisha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku moja baada ya Aksofu Kakobe kukosoa namna serikali inavyotenda mambo yake, akisisitiza kwamba Tanzania si nchi ya chama kimoja kama ambavyo viongozi wanataka kuigeuza na hivyo kuwataka viongozi wa serikali waanze kutubu. Kamugisha amesema kuwa, wao kama viongozi wa CCM hawaweza wakakaa kimya wanapoona chama kinachafuliwa na viongozi wake ambao wanafanya kazi kwa niaba ya watanzania wakikashifiwa. Aidha, alisema kuwa, siasa ni kwa ajili ya wanasiasa, na ...
MTOTO PATRICK WA MUNALOVE NA CASTO AFARIKI DUNIA -VIDEO July 4, 2018 by ATILIO KIBUGA BLOG ATILIO KIBUGA BLOG KY AJK WALTER KIBUGA MSANII wa Filamu za Bongo na mdau wa Muziki wa Bongo Fleva, Rose Alphonce ‘Muna Love’ na mtangazaji Casto Dickson, wamefiwa na mtoto wao aitwaye Patrick ambaye amefariki leo Julai 3, 2018 akiwa nchini Kenya akipatiwa matibabu. Sababu za kifo chake hakijafahamika. Muna Love akiwa na mtoto wake. Kupitia ukurasa wa instagram wa Zamaradi Mketema ameandika “Tumejitahidi ila MUNGU ana mitihani yake, mikono inatetemeka ila ndio ukweli, PATY AMEFARIKI!! Pumzika kwa amani baba”
Comments
Post a Comment