RPC Shanna: Atakaefunga Barabara Na Kuchoma Matairi Mkesha Wa Mwaka Mpya Kukiona SeeBait
Wednesday, December 27, 2017 RPC Shanna: Atakaefunga Barabara Na Kuchoma Matairi Mkesha Wa Mwaka Mpya Kukiona Na Mwamvua Mwinyi,Pwani Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Jonathan Shanna ,ametoa onyo kwa watu wenye tabia ya kufunga barabara kwa kuchoma matairi katika mkesha wa mwaka mpya na kupelekea usumbufu kwa watuamiaji wengine wa barabara kuacha kufanya kitendo hicho . Amesema atakaejaribu kuchoma moto matairi kwenye mkesha huo,jeshi la polisi mkoani hapo litamchukulia hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine. Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya kiusalama inavyoendelea hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye sikukuu ya mwisho wa mwaka ,kamanda Shanna alisema wanazidi kuimarisha doria katika pande zote za mkoa huo. Alisema kipindi cha sikukuu ya x-mas hali ilikuwa shwarii hivyo wanaendelea na misako ya miguu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na doria hizo zitakuwa mtaa kwa mtaa na ...