Hiki ndicho kilipelekea Mourinho na Arteta kupigwa chupa, Mourinho ndio chanzo


Hiki ndicho kilipelekea Mourinho na Arteta kupigwa chupa, Mourinho ndio chanzo


Ha ikuwa rahisi hata kidogo kwa Derby kubwa na ngumu kama ya Manchester kuisha hivi hivi bila kuwa na habari kubwa, na matokeo ya mechi ilikuwa habari iliyotarajiwa kwani mpira wowote lazima kuwe na matokeo.

Habari isiyotarajiwa ni tukio lililotokea baada ya mchezo huo ambapo inadaiwa kocha Jose Mourinho alikuwa chanzo cha fujo kubwa iliyotokea katila vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mchezo huo.

Inadaiwa kwamba wachezaji wa Manchester City walikuwa wakishangilia sana katika vyumba vya kubadilishia nguo huku wakiwa wamefungulia sauti ya mziki kubwa sana kiasi cha kuwasumbua wengine.

Jose Mourinho hakufurahia jambo hilo na aliamua kwenda kuwaambia wapunguze sauti, lakini wakati Mou akiwaambia hivyo kulitokea hali ya majibizano kati ya wachezaji wa Citu wakiongozwa na golikipa Ederson na kocha huyo wa United.

Inadaiwa Ederson alikuwa akibishana na Mourinho na wakati wakiendelea kubishana ndipo kulirushwa kopo la maji ambalo halikumpata vizuri Mourinho na baadae watu wa usalama walituliza hali hiyo.

Lakini katika tukio lingine Mikel Arteta alionekana akitokwa na damu baada ya kupigwa na chupa, huku baadhi ya mashahidi waliokuwa katika tukio hilo wakidai kwamba Lukaku alikuwa karibu na eneo ambalo Arteta alipigwa chupa na inawezekana ndiye aliyeirusha.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUFUNGUA BLOG KWENYE BLOGGER

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2017 HAYA HAPA

FAIDA NA MAAJABU JUISI YA UBUYU