Bei Mpya Ya Mafuta Kwa Mwezi Wa Disemba
Tuesday, December 12, 2017
Bei Mpya Ya Mafuta Kwa Mwezi Wa Disemba
MAMLAKA ya udhibiti wa huduma za nishati na maji( ZURA ) imetoa taarifa juu ya bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika rasmi kuanzia leo Jumanne tarehe 12-12-2017.
Akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Maisara Kaimu Mkurugenzi masuala ya wateja Mussa Ramadhani Haji alisema kuwa bei hizo Zura imepanga kufuatia mambo yafuatayo;-
Wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta Duniani (Platts Quatations) katika mwezi wa Novemba 2017 , kwa lengo la kupata kianzio cha kufanyia mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi wa Disemba 2017.
Pia thamani ya shillingi ya Tanzania , gharama za usafiri , Bima na’ Premium ‘hadi Zanzibar . Kodi za serikali na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja.
Alisema bei za rejereja ya mafuta ya Petroli kwa mwezi wa Disemba, 2017 imepanda kwa shillingi (100) kwa lita kutoka shilling 2,130 Mwezi wa Novemba , 2017 hadi shilling 2,230 kwa lita katika mwezi wa Disemba , 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.5%.
Pia alisema bei ya rejereja ya mafuta ya Dizeli kwa Mwezi wa Disemba , 2017 imeshuka kwa shilling (90) kwa lita kutoka shilling 2,280 kwa lita katika mwezi Novemba hadi shilling 2,190 kwa lita katika mwezi wa Disemba, 2017 sawa na asilimia 4%.
Aidha alisema bei ya reja reja ya mafuta ya Taa kwa mwezi wa Disemb 2017 imepanda kwa shilling (80) kwa lita kutoka shillingi 1.539 kwa lita katika mwezi wa Novemba , 2017 hadi shilling 1,619 katika mwezi wa Disemba , 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.9%
Vilevile bei ya reja reja ya mafuta ya Banka kwa mwezi waDisemba, 2017 imeshuka kwa shilling (90) kwa lita kutoka shillingi 2,122 kwa lita katika mwezi wa Novemba, 2017 hadi shilling 2,032 katika mwezi wa Disemba , 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.4%.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
Comments
Post a Comment