Pierre-Emerick Aubameyang: Mwafrika anayevuma Ujerumani
Pierre-Emerick Aubameyang: Mwafrika anayevuma Ujerumani
Hakuna mara hata moja katika historia ndefu ya ligi kuu wa Ujerumani Bundesliga ambapo mchezaji kutoka Afrika alikuwa ameongoza kwa ufungaji wa mabao ligini peke yake hadi pale Pierre-Emerick Aubameyang alipofunga mabao 31 msimu wa 2016-17.
Idadi yake ya mabao ilimuwezesha raia huyo wa Gabon kuvunja hata rekodi iliyowekwa na mchezaji wa Ghana Tony Yeboah, ambaye alimaliza akiwa anashikilia nafasi ya ufungaji mabao ligini na mchezaji mwingine miaka ya 1990.
Kadhalika, ilikuwa ni mara ya nne kwa mchezaji kufunga Zaidi ya mabao 30 katika msimu mmoja Bundesliha - na mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 40.
Jambo la kufurahisha pia ni hali kwamba nyota huyo wa Dortmund alikuwa amefunga mabao yake 31 kutoka wka mechi 32 pekee. Kama mchezaji mwenye kasi ajabu na uwezo wa kufunga mabao, hilo lilimshindia nafasi katika kikosi bora cha mwaka Bundesliga kwa mwaka wa pili mtawalia.
Mabao matatu aliyoyafunga dhidi ya Benfica mwezi Machi yalimsaidia kufikisha magoli 40 kwa jumla, moja ambalo liliwasaidia Dortmund kushinda fainali ya Kombe la Ujerumani kwa kuwalaza
Aubameyang alikuwa anacheza vizuri sana kiasi kwamba aliteuliwa kushindania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka duniani ya Fifa - Mwafrika pekee kuteuliwa kushindania tuzo hiyo.
Mchezaji huyo wa miaka 28 alikuwa pia, pamoja na mchezaji mwingine anayeshindania Tuzo ya Mwanakandanda Bora wa Afrika ya BBC Sadio Mane, kwenye orodha ya waliokuwa wanashindania tuzo ya Ballon d'Or.
Licha ya matarajio mengi kwamba mchezaji huyo wa Gabon anayependa maisha ya kifahari angeondoka Dortmund kabla ya msimu kuanza, hilo halikutimia.
Klabu za ngazi ya juu kama vile Paris Saint-Germain na Manchester City zilitaka kumnunua lakini ndoto yake ya muda mrefu, ambayo inafahamika hadharani, ya kujiunga na Real Madrid ilikufa klabu hiyo anayoipenda sana babu yake Aubameyang ilipoacha kumtafuta licha ya ufungaji wake mzuri wa mabao tangu alipojiunga na Dortmund mwaka 2013.
Kwa kweli, mabao yake 135 kutoka kwa mechi 204 kufikia wakati wa kuchapishwa kwa Makala hii, yana maana kwamba anaweza kufunja rekodi ya ufungaji mabao katika historia ya Borussia Dortmund kufikia mwisho wa mwaka ujao. Rekodi ya sasa iliwekwa na Michael Zorc.
'Auba' aliendeleza msimu mpya pale alipoachia ule uliopita - akitumia kasi yake na ufasaha kwenye goli kufunga mabao manane katika mechi sita za kwanza za ligi.
Kimataifa, nahodha huyo wa Gabon atataka kuusahau mwaka huu - hakufanikiwa sana na klabu yake ilikuwa taifa la nne mwenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika kuondolewa kwenye michuano hatua ya makundi. Hii ni licha yake kuwafungia mabao mawili katika mechi tatu.
Kwa hivyo, ufanisi wake Ujerumani utamfanya Aubameyang kuwa raia wa kwanza wa Gabon kushinda tuzo hii ya BBC?
Comments
Post a Comment